KISWAHILI

 

SWAHILI

KANISA LA MTAKATIFU RUDE

Rude” au “Rood” ni neno medieval cha kale likimaanisha Kusulubiwa Msalabani.

Kanisa la kwanza kwenye tovuti hii/eneo hili lilianzishwa na Mfalme Daudi wa Kwanza katika mwaka 1129, lakini likateketezwa kwa moto mwaka 1406. Muda mfupi baadaye, Bwana Chamberlain wa Scotland alitoa msaada wa kujenga kanisa jipya; ambapo sehemu ya kuabudia kanisani, sehemu ya ibada upande wa kusini wa mnara vyote vilikamilika mwaka 1414. Hii sehemu ya Kanisa ambayo ina nguzo za mviringo na pembe za mduara za Kiskotish, ndio yenye paa la mbao linaloonekana hadi leo ingawa mabadiliko mengi yamefanyika.

Kwa sababu Kanisa halikuwa na ukubwa wa kutosha usharika, sehemu ya kwaya (au sehemu ya mashariki) ilijengwa kati ya 1507 na 1546 ikiwa ni matokeo ya hamasa ya wafanyabiashara chini ya uongozi wa bwana Yohana Coutts, mtu ambaye aliunganisha wenzie kuwa na mafanikio.

Kufuatia ugomvi baina ya viongozi (mawaziri) wawili wa Kanisa na wafuasi wao, katika mwaka 1656 halmashauri ya mji ikagawanywa na mahali hapo pakajengwa msalaba (ambapo ndipo ulipo hadi leo). Kutokana na mabadiliko haya pakatokea makanisa mawili: Kanisa la Mashariki na Kanisa la Magharibi, kila kanisa na kiongozi wake. Hali hii iliendelea hadi 1935, wakati sharika mbili zilipoungana chini ya kiongozi mmoja wa kanisa.

Kufuatia matengenezo makubwa kati ya mwaka 1936 na 1940, ukuta uliokuwa unayagawa makanisa haya mawili uliondolewa na kuta fupi mbili zilipanuliwa na paa la kuunganisha haya makanisa lilijengwa na mahali pa kufanyia vikao vya viongozi wa kanisa vilijengwa ndani ya jengo la Kwaya.

Kati ya 1965 na 1968 yalifanyika marekebisho zaidi nje. Hii ilihusisha uwekaji wa madirisha na ubadilishaji wa mawe yaloharibika, na urekebishaji wa mfumo mzima wa ujenzi wa mawe na ufufuaji wa mfumo wa kuleta joto ndani ya nyumba. Mwaka 1970 ujenzi wa mnara wa kengele na upachikaji wa kengele 6 ulifanyika. Hizi kengele zinaweza kupigwa kwa mikono au kwa kutumia vifaa maalum. Kati ya 1987 na 1993 ukarabati mkubwa wa kanisa ulifanyika kwa gharama ya Paundi za Uingereza 1,250,000 (£1,250,000).

Maria, Malkia Skotland, aliabuda katika Kanisa hili na John Knox alihubiri hapa. Aliyekuwa mtoto mdogo wa Maria akiitwa James wa Sita wa Uskoti, ambaye baadaye akawa James wa kwanza wa Uingereza katika mwaka 1603, baada ya kifo cha Malkia Elizabeth, alipata taji la ufaime hapa tarehe 29 Julai 1567, na kufanya Kanisa hili kuwa Kanisa pekee Uingereza, katika matumizi ya kawaida ya ibada, ukiachilia mbali kanisa la Westminster Abbey jijini London ambapo usimikaji wa mfalme/malkia hufanyika.


TAFADHALI USIONDOE HII KUTOKA KANISANI

www.holyrude.org tom.buchanan@talktalk.net